tonestro Anza sasa
Mwanamke mwenye nywele fupi nyekundu amesimama nyumbani na saksafoni yake ya alto, simu kwenye stendi kando yake

Jifunze saksafoni. tonestro inasikiliza.

Wimbo wako wa kwanza ndani ya dakika 10. Kwenye saksafoni yako mwenyewe.

Anza sasa Siku 7 bila malipo · iOS na Android
App of the Day kwenye App Store Vipakuliwa
zaidi ya milioni 1

Unapiga. tonestro inasikia kila noti.

Kila noti, kwa sauti sahihi na kwa wakati sahihi. Ukikosea moja, tonestro inaisikia papo hapo.

Mwanamume anatabasamu nyumbani akiwa na saksafoni yake, kompyuta kibao kwenye stendi mbele yake

Jifunze saksafoni, hatua kwa hatua.

Kozi zilizoandaliwa na walimu wa muziki zinakupeleka kuanzia noti zako za kwanza hadi nyimbo zako za kwanza, nyingi zikiwa na muziki wa kusindikiza.

  • Alto, tenor, soprano, baritone tonestro inasikiliza zote nne.
  • Chati ya vidole Kila mkao wa vidole, ndani ya programu.
  • Punguza kasi Fanya mazoezi ya sehemu ngumu kwa kasi ya 80% au 60%.
Kozi ya saksafoni ndani ya tonestro: noti yako ya kwanza, melodi yako ya kwanza, kupiga pamoja na bendi

Hujachelewa kuanza.

  • Hujawahi kupiga? Anza na noti zako za kwanza na wimbo wako wa kwanza.
  • Ulipiga shuleni? Chagua kozi yako na uendelee pale ulipoachia.
Mwanamume anatabasamu sebuleni kwake akiwa na saksafoni yake, stendi ya nota kando yake

Kuanza kujifunza saksafoni

Watu wazima wengi huanza saksafoni kwa sababu ya sauti moja wanayoipenda. Noti za kwanza zinakuja haraka; kupiga kwa sauti sahihi na kwa mdundo thabiti ndicho kinachohitaji mazoezi. tonestro inasikiliza kila noti na kukuonyesha papo hapo kipi kilikuwa sahihi.

Fanya mazoezi kwa dakika chache karibu kila siku na upe midomo yako muda wa kupata nguvu. Punguza kasi ya sehemu, ipige vizuri, kisha ongeza kasi.

tonestro inafanya kazi na saksafoni ya alto, tenor, soprano na baritone.

Unachohitaji

  • Saksafoni yako mwenyewe: alto, tenor, soprano au baritone
  • Vilimi vichache (reeds)
  • iPhone, iPad au simu ya Android yenye muunganisho wa intaneti

Si kwa ajili yako tu. Ni kwa familia nzima.

Mpango mmoja kwa hadi watu sita. Kila mtu anachagua ala yake.

Tazama Mpango wa Familia
Msichana anapiga saksafoni huku baba yake akimtazama na kutabasamu, kompyuta kibao kwenye stendi mbele yao

Maswali kuhusu kujifunza saksafoni

Je, saksafoni ni ala nzuri ya kuanza nayo ukiwa mtu mzima?

Ndiyo. Watu wazima wengi huanza saksafoni bila uzoefu wowote. tonestro inakwenda hatua kwa hatua na inasikiliza kila noti unayopiga.

Ninaweza kutumia saksafoni gani?

Alto, tenor, soprano au baritone. tonestro inafanya kazi na zote nne.

Je, kuna chati ya vidole?

Ndiyo. Chati ya vidole imo ndani ya programu, kwa hiyo unaweza kuangalia kila noti unapofanya mazoezi.

Je, ninahitaji kujua kusoma noti?

Hapana. Kozi zinakufundisha kusoma noti unapopiga, na unaweza kuonyesha majina ya noti unapojifunza.

Nitapiga wimbo wangu wa kwanza kwenye saksafoni lini?

Ndani ya dakika 10 za kwanza. Unapiga noti moja au mbili pamoja na wimbo halisi na bendi: kidogo mwanzoni, lakini ni muziki halisi. Kasi kamili itakuja baadaye, kadiri sauti yako inavyokua.

Ninaweza kutumia vifaa gani?

Masomo ya saksafoni yanafanya kazi kwenye iPhone na iPad (iOS 15 au toleo jipya zaidi) na kwenye simu za Android (Android 8 au toleo jipya zaidi, kumbukumbu ya angalau GB 4). tonestro inahitaji muunganisho wa intaneti.

Inagharimu kiasi gani?

Unaweza kujaribu tonestro bila malipo kwa siku 7 ukichagua mpango wa mwaka. Programu inakuonyesha bei kabla hujanunua. Ukighairi angalau saa 24 kabla ya jaribio kuisha, hutatozwa chochote. Unaweza kughairi ndani ya programu kupitia Profile → Settings → Manage Subscription.

Au jifunze ala nyingine

Ndani ya dakika 10 utapiga wimbo wako wa kwanza.

Pakua tonestro kwenye App Store Pata tonestro kwenye Google Play

Siku 7 bila malipo

Wimbo wako wa kwanza ndani ya dakika kumi

Changanua msimbo kwa kamera ya simu yako ili upate programu.

Pakua tonestro kwenye App Store Pata tonestro kwenye Google Play

Siku 7 bila malipo